IQNA

Muqawama

Afisa wa PMU ya Iraq: Mashahidi Soleimani, Al-Muhandis waliushinda ugaidi wa kimataifa

17:23 - January 08, 2024
Habari ID: 3478166
IQNA - Makamanda wa harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis walikuwa wapiganaji wakubwa waliopata ushindi dhidi ya ugaidi wa kimataifa.

Haya ni kwa mujibu wa Muhand Najm Abd al-Aqabi, mkurugenzi wa ofisi ya mahusiano ya umma ya Hashd al-Shaabi ya Iraq, yaani Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi (PMU). Ameyasema hayo kwenye warsha iliyofanyika kwa njia ya intaneti au webinar ambayo mada yake kuu ilikuwa ni: "Utandawazi wa Muqawam; Mafanikio ya Itikadi ya Shahidi Soleimani. Webinar hiyo iliandaliwa na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) siku ya Jumatatu.

"Jukumu la Shahidi Soleimani katika kufufua safu ya muqawama na kuigeuza kuwa nguvu ya kikanda na kimataifa," na "athari za Jenerali Soleimani na itikadi yake katika kuleta mabadiliko katika mpangilio wa ulimwengu wa sasa na mpito kuelekea mpangilio mpya wa ulimwengu" zilikuwa mada kuu mbili za warsha hiyo ya mtandaoni.

Warsha hiyo pia ilihutubiwa na Abu Samir Musa, mwanachama mwandamizi wa harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina, Sheikh Qazi Yusuf Hunaina, Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, na Abu Wassam Mahfouz Munawwar, mkuu wa ofisi ya uhusiano wa kigeni wa harakati ya Jihad ya Kiislamu.

Jenerali Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), na al-Muhandis, naibu mkuu wa PMU ya Iraq, pamoja na baadhi ya wanajihadi wenzao, waliuawa katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za jeshi la kigaidi la Marekani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad Januari 3, 2020.

Katika hotuba yake, al-Aqabi alisema kwamba haijalishi ni kiasi gani kitasemwa au kuandikwa kuhusu Mashahidi Soleimani na al-Muhandis, haitatosha kufafanua juu ya sehemu ndogo ya kile ambacho makamanda hao wawili wa muqawama waliufanyia ulimwengu wa Kiislamu, mataifa yanayodhulumiwa, na kwa ubinadamu kwa ujumla.

Walichofanya kilivuka ulimwengu wa Kiislamu na mataifa ya Kiislamu, alisisitiza, akiongeza kuwa walitumikia wasio Waislamu kama Wakristo, Waizadi , na wengine, haswa huko Iraqi.

Al-Aqabi amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel walidhani kwamba kwa kuuawa shahidi Jenerali Soleimani na al-MUhandis, harakazi za mapambano ya Kiislamu zitaporomoka lakini kinyume chake, mauaji yao yaliimarisha zaidi muqawama na kupelekea kuenea kwake zaidi miongoni mwa watu katika nchi za Kiislamu. .

Ama kuhusu Iraq, kuuawa shahidi kamanda huyo wa muqawama wa pande mbili kumeifanya nchi hiyo kuwa na nguvu na azma zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi na kuongeza kuwa, kumezidisha chuki za wananchi wa Iraq dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni.

Zaidi ya hayo, kifo chao kiliifanya PMU kuwa na nguvu zaidi, alisema. "Kabla ya wao kuuawa makamanda hao, tulikuwa na wanachama 200,000 katika PMU lakini leo na katika wakati huu, tunazungumza juu ya wapiganaji zaidi ya milioni 2.5."

Akiashiria umaarufu wa mashahidi hao wawili, alisema sherehe za kuwakumbuka zilianza wiki tatu zilizopita bado zinaendelea nchini Iraq.

Al-Aqabi pia ameashiria kuongezeka sauti ya muqawama katika eneo na dunia kufuatia kuuawa shahidi Jenerali Soleimani na al-Muhandis akisema sauti ya Ghaza na Palestina ni kubwa kuliko ile ya utawala wa Kizayuni, Marekani na waitifaki wao hivi leo.

3486730

 

captcha