Kituo hicho kilitangaza utayari wake wa kuandaa kuandaa hafla kadhaa katika siku hiyo, ambayo inaangukia tarehe 27 ya mwezi wa Hijri wa Rajab. Mkuu wa kituo hicho Sheikh Khairuddin al-Hadi alisema kwamba mada za hafla hii zinawakilisha ujumbe wa ulimwengu wa Qur’ani. Alisema kutakuwa na mfululizo wa shughuli zitakazofanyika kwa muda wa siku saba katika eneo la Bain al-Haramayan (eneo kati ya Haram mbili takatifu za Imam Hussein na Hadhrat Abbas) na kote katika majimbo yote ya Iraq. Kuzindua Encyclopedia ya Mafundisho ya Qur’ani ya Ahl-ul-Bayt (AS) ni miongoni mwa shughuli hizi, alibainisha.
Sheikh al-Hadi aliongeza kwamba mkutano wa sita wa kimataifa wa Qur’ani pia utafanyika kwa kuzingatia urithi wa Qur’ani wa Imam Hussein (AS) na Ahl-ul-Bayt (AS). Pia kutakuwa na maonyesho ya kimataifa ya Qur’ani kwa ushiriki wa taasisi za Iraq na kimataifa, aliendelea kusema.
Mbali na kuandaa mikutano ya kitaifa na kimataifa ya Quran inayotilia mkazo umuhimu wa shughuli za Qur’ani, semina za kitaaluma na mijadala maalum itafanyika kushughulikia changamoto, alisema. Mpango huu wa maadhimisho ya Siku ya Qur’an unatekelezwa chini ya usimamizi wa moja kwa moja na msaada wa Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, mwakilishi wa Marjaa Taqlid, na Hassan Rashid Abayji, katibu mkuu wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) kwa lengo la kufanya siku hiyo kuwa fursa ya kuonyesha ukuu wa ujumbe wa Qur’ani na kufikia hatua ya juu katika shughuli za Quran katika ngazi za kitaifa na kimataifa, alihitimisha.
3491220