Mashindano hayo yatapangwa kwa ushirikiano na mashirika ya Wakfu ya Shia na Sunni nchini Iraq. Washindani watashindana katika kategoria za kuhifadhi na usomaji wa Qur’ani Tukufu. Kikao cha kamati ya kiufundi ya mashirika ya Wakfu ya Shia na Sunni kilifanyika mjini Baghdad mapema wiki hii.
Baadhi ya maafisa wa kidini na wa Qur'ani na watu mashuhuri wa nchi hiyo pia walihudhuria mkutano huo. Walijadili maandalizi muhimu ya mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani.
Toleo la kwanza la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani la Iraq lilikuwa limepangwa kufanyika mapema 2024 lakini liliahirishwa kwa sababu kadhaa
Shughuli za Qur'ani zimeendelea kwa kiasi kikubwa nchini Iraq tangu kupinduliwa kwa dikteta wa zamani Saddam Hussein mwaka 2003.
Kumekuwa na mwelekeo unaokua wa programu za Qur'ani kama vile mashindano, vipindi vya kisomo na programu za elimu zilizofanyika nchini katika miaka ya hivi karibuni.
.