IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu

Qiraa ya hivi karibuni ya Ustadh Mahmoud Shahat Anwar

TEHRAN (IQNA)- Mahmoud Shahat Anwar, msomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu nchini Misri hivi karibuni alisoma aya za 24-25 za Surah Baqarah alipokuwa akihudhuria mkutano wa Qur'ani wa mkoa wa Qalubiyeh wa nchi hii.

Qiraa ya aya hizo ilifanyika tarehe 15 Mei mwaka  katika kijiji cha "Basous" katika mkoa wa Qalubiyeh, Misri.

“Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walio andaliwa hao wanao kanusha.  Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapo pewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyo fanana; na humo watakuwa na wake walio takasika; na wao humo watadumu."