Katika klipu hii, anaseoma Aya ya 59 ya Surah Al-An’am: “Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha"
Anwar Shahat Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1979. Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Iraq, Iran, Qatar, UAE, Algeria, Syria, Pakistan, Afrika Kusini, Ugiriki, Uturuki na Ubelgiji.