IQNA

Qari wa Misri, Ustadh Anwar akisoma aya katika Sura Al Fajr

Katika riwaya tofauti, Maimamu wa Masoumin (AS) wameinasibisha Sura ya “Al Fajr” na Imam Husein (AS); Kwa msingi wa kwamba kuinuka na kuuawa kishahidi kwa Mtukufu Huyo kumekuwa ni kama wakati wa kuwadia Alfajiri baada ya kiza cha usiku. Katika mwezi wa Muharram na katika siku za maombolezo ya kiongozi wa mashahidi, Hadhrat Aba Abdullah Al-Hussein (AS), IQNA husambaza airaa za Sura Al Fajr kwa sauti za wasomaji mashuhuri duniani, wa kimataifa na mashuhuri wa nchi. Hapa basi utasikia kisomo cha mkusanyiko wa aya ya 17 hadi mwisho katika Sura Fajr kwa sauti ya Shahat Mohammad Anwar, msomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu nchini Misri.

 

 

 

 

 

 

      17.Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, 

  1. Wala hamhimizani kulisha masikini; 
  2. Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, 
  3. Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. 
  4. Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, 
  5. Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, 
  6. Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? 
  7. Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! 
  8. Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. 
  9. Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. 
  10. Ewe nafsi iliyo tua! 
  11. Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. 
  12. Basi ingia miongoni mwa waja wangu, 
  13. Na ingia katika Pepo yangu.