IQNA

Siku ya Mwisho ya Mashindano ya 46 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran

Bojnourd (IQNA) – Washiriki wa kategoria za usomaji na kuhifadhi Qur’ani kwa wanaume walipanda jukwaani Ijumaa ambayo ilikuwa siku ya mwisho ya Mashindano ya 46 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran. Mashindano hayo yalianza Desemba 1 huko Bojnourd, Mkoa wa Khorasan Kaskazini, na kukamilika baada ya siku nane kwa kutangazwa washindi wake Jumamosi.