Tarehe 10 Rajab miaka 1250 iliyopita, alizaliwa Imam Muhammad Taqi mmoja wa watu wa Nyumba Tukufu ya Bwana Mtume SAW katika mji mtakatifu wa Madina.
Imam Taqi Al-Jawad (as) alichukua jukumu la kuongoza Umma wa Kiislamu baada ya kuuawa shahidi baba yake yaani Imam Ridha (AS). Mtukufu huyo alikuwa maarufu kwa lakabu ya 'Jawad' yenye maana ya mtu mkarimu mno, kutokana na ukarimu wake mkubwa.
Source: news.razavi.ir