IQNA

Kikao cha kufundisha Qur'ani katika ukumbi wa Zoorkhaneh + Picha na Video

Kikao cha mafunzo ya Qur'ani Tukufu cha Javad Panahi, qari na mwalimu wa kimataifa wa Qur'ani wa Iran, kilifanyika katika moja ya Zoorkhane huko Mashhad, ambapo maashiqi wa Qur'ani Tukufu walihudhuria.
Zoorkhaneh ni moja wapo ya michezo ya kitamaduni ya Iran. Ukumbi wa Zoorkhaneh ni mahali ambapo wanafanyia mchezo huu.  Zoorkhane sio tu mahali pa mafunzo na kufanya michezo ya kale, lakini pia ni kituo cha  mafundisho ya kimaadili na kiroho na hivyo ni mahali pnye heshima kubwa.