IQNA

Qari wa Iran akisoma aya za Qur'ani kuhusu Mwokozi anayesubiriwa

IQNA - Katika video aliyeirekodi maalumu kwa ajili ya IQNA, qari wa Iran Hamed Valizadeh amesoma aya mbili zinazohusu ujio wa Mwokozi.

Alisoma aya ya 5 ya Surah Al-Qasas na 105 ya Surah Al-Anbiya.

Aya ya 5 ya Sura Al-Qasas: “Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi."

Aya ya 105 ya Surah Al-Anbiya: “Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema."