IQNA

Tamthilia ya Ta’zieh nchini Iran katika mkoa wa Fars

IQNA - Onyesho kubwa zaidi la tamthilia ya Ta’zieh lilifanyika katika kijiji karibu na jiji la Fasa, Mkoa wa Fars, Julai 18, 2024, mwaka huu.

Ta’zieh ni onyesho la tamthilia linalosimulia matukio yaliyotokea wakati wa Vita 

 vya Karbala mwaka 61 Hijria

Inalenga kumkumbuka masaibu ya Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa Shia.

Imam Hussein (AS) , mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), na masahaba zake 72 watiifu, waliuawa shahidi siku ya Ashura katika vita vya Karbala dhidi ya Khalifa wa pili wa Bani Umayya, Yazid .
 Imam Hussein (AS) aliuawa baada ya kukataa kuahidi utii kwa mtawala dhalimu.

Taratibu za Ta’zieh zinaashiria msimamo wa milele na usioyumba wa ukweli dhidi ya uongo na mapambano ya binadamu dhidi ya dhulma. 
Ta’zieh ilisajiliwa katika orodha ya UNESCO ya Turathi za Utamaduni Zisizogusika za Binadamu mwaka wa 2011.