IQNA

Kisomo cha Mbinguni: Msikilize Qari Shaban Sayyad akisoma aya za Surah Al-Fath

IQNA-Ifuatauo ni qiraa ya aya ya 29 ya Surah Al-Fath ikisomwa na Qari Shaban Abdul Aziz Sayyad wa Misri.

Mtume Muhammad (SAW) alisema wakati mmoja kwamba kuisikiliza Qur'ani Tukufu humletea mja thawabu za Mwenyezi Mungu, huku kila herufi ikisikika ikistahiki tendo jema kwa msikilizaji, na kumpandisha msikilizaji katika safu ya wale wanaosoma maandiko matukufu na kupaa kuelekea mbinguni. 
Shirika la habari la IQNA limeratibu na kutoa mfululizo unaoitwa "Kisomo cha Mbinguni," wenye kumbukumbu za kuvutia za wasomaji maarufu Qur’ani Tukufu.