IQNA

Majeshi ya Yemen yatekeleza oparesheni iliyofanikiwa dhidi ya Saudia

15:23 - June 23, 2020
Habari ID: 3472891
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Majeshi ya Yemen amesema majeshi ya nchi hiyo yametekeleza oparesheni maalumu ndani kabisa ya ardhi ya Saudi Arabia.

Katika taarifa siku ya Jumanne, Msemaji wa Majeshi ya Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree alitangaza kuwa, mapema leo asubuhi majeshi ya Yemen yametekeleza oparesheni ya mashambulizi kwa makombora ambayo yamelenga vituo vya kijeshi katika mji mkuu wa Saudia, Riyadh. Aidha amesema katika oparesheni hiyo vituo  vingine vya kijeshi vimelengwa  katika maeneo ya Jizan na Najran.

Msemaji wa Majeshi ya Yemen amesema katika oparesheni hiyo makombora ya balistiki na cruise aina ya 'Quds' an 'Dhulfiqar' na ndege zisizo na rubani au drone zimetumika kushambulia vituo vya kadhaa vya kijeshi Saudia.

Yahya Saree amesisitiza kuwa oparesheni hiyo ambayo ni ya nne ya aina yake imetekelezwa katika kujibu hujuma ya kijeshi Saudia dhidi ya taifa la Yemen. Halikadhlika amesema oparesheni hiyo pia ni jibu kwa mzingiro wa kidhalimu wa Saudia dhidi wananchi wa Yemen na kuongeza kuwa, maadamu Saudia inaendeleza uhasama na uvamizi wake, oparesheni kali zaidi zitatkelezwa.

Wanaharakati nchini Saudia leo wameripoti kusikia milipuko mikubwa kaskazini mwa mji mkuu, Riyadh. Saudia imedai kuwa imeangusha makombora ya balistiki yaliyovurumishwa na Harakati ya Ansarullah.

Majeshi ya Yemen mara kwa mara hutekeleza oparesheni za kulipiza kisasi dhidi ya Saudia kutokana na jinai zinazotekeleza na muungano wa ufalme huo dhidi ya raia wa Yemen.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. 

Kituo cha Haki za Binadamu cha Ainul Insaniya kutoa ripoti na kutangaza kuwa, tokea muungano wa Saudia uanzishe vita dhidi ya Yemen mnamo Machi 26, 2015 hadi sasa, watu 16, 672 wamepoteza maisha moja kwa moja kutokana na vita hivyo na miongoni mwao kuna watoto 3,742 na wanawake 2,364.

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3906467/

Kishikizo: yemen saudia ansarullah
captcha