IQNA

Wayemen walaani muungano wa Saudia kwa kutumia mabomu ya vishada

22:27 - June 11, 2020
Habari ID: 3472857
TEHRAN (IQNA) –Wayemen wamelaani muungaji wa kivita unaaongozwa na Saudia kwa kutumia mabomu vya vishada dhidi ya eneo la makazi ya raia katika mji mkuu, Sana’a na kupelekea familia moja kujeruhiwa vibaya.

Katika taarifa, Wizara ya Haki za Binadamu ya Yemen imetahadahrisha kuwa mabomu ya vishada ni hatari kwa raia hasa wanawake na watoto iwapo watakaribia mabomu hayo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa muungano huo wa Saudia umetumia maelfu ya mabomu ya vishada katika maeneo ya raia ambapo wengi wameuawa na kujeruhiwa. Mabomu mengi ya vishada hayalipuki na hivyo huwa hatari kwa raia.

Utumizi wa mabomu ya vishada (cluster bombs) ni marufuku kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasio na hatia. Zaidi ya watu 17,000 wanaripotiwa kupoteza maisha moja kwa moja  katika vita vya Saudia dhidi ya Yemen huku makumi ya maelfu yaw engine wakipoteza maisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3471666

Kishikizo: yemen mabomu vishada saudia
captcha