IQNA

13:52 - June 29, 2020
News ID: 3472911
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa Maulamaa wa Kiislamu (IUMS) ametahadharisha kuhusu njama hatari inayopangwa dhidi ya Yemen na ametaka nchi hiyo inusuriwe.

Sheikh Ali Mohiuddin Al-Qaradaghi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa Maulamaa wa Waislamu ametoa taarifa na kusema: "Baadhi wanataka Yemen iliyokuwa na ufanisi ibadilike na kuwa nchi yenye hali mbaya zaidi. Wanataka kuigawa Yemen vipande vipande na wanataka Wayemen wazame katika umasikini na vita ili waweze kuwahibiti."

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa Maulamaa wa Waislamu meongeza kuwa, iwapo nchini Yemen hakutakuwa na watu wenye busara ambao watadiriki njama hii na kukabiliana nayo haraka, basi nchi hiyo itakumbwa na hali mbaya sana.

Sheikh Al-Qaradaghi ameendelea kwa kuashiria njama ambazo Saudi Arabia inatekeleza kimataifa na kusema Saudia inachochea hitilafu ndani ya Yemen na sasa uchumi wa nchi hiyo unaelekea kuangamia kikamilifu. Kwa msingi huo, Sheikh Al-Qaradaghi amesema watu wenye busara na tadibiri nchini Yemen wanatarajiwa kuchukua hatua za haraka bila kupoteza wakati ili waliende nchi yao.

Mwanazuoni huyo mwandamizi amesema ni wajibu wa kisheria kuwasaidia watu wa Yemen waondokane na hali ya sasa.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Baraza la Mpito la Kusini mwa Yemen, ambalo linapata himaya ya Umoja wa Falme za Kiarbau, mnamo Juni 19 liliuteka mji wa Hadibu ambao ni mji mkuu wa Kisiwa cha Socotra baada ya mapigano makali na vikosi vya serikali.  Hatua hiyo imetajwa kuwa ni katika njama iliyoratibiwa kwa kuigawa Yemen kuwa nchi mbili, moja ya kusini na nyingine ya kaskazini katika kipindi hiki ambacho muungano wa kijeshi wa Saudia ungali unaendeleza hujuma dhidi ya nchi hiyo.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. 

Kituo cha Haki za Binadamu cha Ainul Insaniya kutoa ripoti na kutangaza kuwa, tokea muungano wa Saudia uanzishe vita dhidi ya Yemen mnamo Machi 26, 2015 hadi sasa, watu 16, 672 wamepoteza maisha moja kwa moja kutokana na vita hivyo na miongoni mwao kuna watoto 3,742 na wanawake 2,364.

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3907535

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: