Fadhila na shaksia ya Imam Ali (as) itabainishwa na kuarifishwa katika kikao maalumu kilichopangwa kufanyika hapo siku ya Jumatatu Juni Nne katika Kituo cha Rasul al-Akram mjini Antananarivo nchini Madagascar, kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Imam huyo mtukufu (as).
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Ismail Pirniya, mwakilisi wa Jamiatul Mustafa (saw) al-Aalamiya nchini Madagascar. Amesema wanafunzi wa masomo ya kidini katika Madrasa ya Imam Swadiq (as), Madrasa ya Tahura na Dar al-Hikma pamoja na wafuasi wa Ahlul Beit (as) mjini humo watashiriki katika kikao hicho kitakaachoanza saa tatu asubuhi na kumalizika kabla ya swala ya Adhuhuri. Sheikh Pirniya atawahutubia hadhirina kuhusiana na uzawa, maisha, ukhalifa na kuuawa shahidi Imam huyo wa kwanza wa Waislamu na kisha kujibu maswali kuhusiana naye. Mashekhe wengine watakaozungumza katika kikao hicho ni pamoja na Salim Ali Yusuf mmoja wa walimu mashuhuri wa Madrasa ya Imam Swadiq (as) na Rijal Natofa mmoja wa walimu wa Kituo cha Kiislamu cha Rasul al-Akram (saw). Amesema mashindano kuhusiana na masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho yatafanyika na kisha washindi 10 kupewa zawadi. Kundi la Kasida la al-Mustafa (saw) litaimba kasida za kumsifu Imam Ali na Ahlul Beit (as) kwa ujumla. 1020345