Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Iraq, ofisi hiyo ilitoa tamko rasmi ikieleza kuwa hakuna ruhusa iliyotolewa kwa ajili ya kuandaa hafla za maombolezo kwa mke wa Ayatullah Sistani katika mikoa ya Iraq isipokuwa Najaf.
"Tunawaarifu ndugu zetu wote wapendwa kuwa hakuna ruhusa iliyotolewa katika mikoa ya Iraq kwa ajili ya kuandaa hafla za maombolezo kwa mama aliyefariki hivi karibuni (Mwenyezi Mungu amrehemu), mke mheshimiwa wa Ayatullah Mkuu Ali al-Sistani," ilisema taarifa hiyo.
Mke wa Ayatullah Sistani alifariki Jumapili jioni baada ya kuugua. Mazishi yake yalifanyika Jumatatu na mwili wake ulizikwa katika Msikiti wa Sheikh Tusi.
Baada ya kifo chake, viongozi wa juu wa kisiasa kutoka Iraq na mataifa mengine, wakiwemo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei, Rais wa Iran, Spika wa Bunge, na wanazuoni wa vyuo vya kidini walitoa salamu za rambirambi kwa Ayatollah Sistani na familia yake.
3494830