Kikao hicho kitafanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Imam huyo mtukufu (saw). Lengo la kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Jumuiya ya Ja'fari ya eneo la Zangipur limetajwa kuwa ni kuwabainishia wakazi wa jimbo hilo shakhsia ya Imam Hussein (as).
Watu watakaozungumza katika kikao hicho ni pamoja na Hujjatul Islam Dhulfiqar Ali mmoja wa wanafunzi wa Jamiatul Mustafa (saw) al-Alamiya.
Washairi mashuhuri wa India wamealikwa kushiriki katika kikao hicho kwa kusoma mashairi ya kumsifu Imam Hussein (as). 1032874