Semina hiyo iliyoanza siku ya Jumamosi na kumalizika Jumatatu tarehe 18 Juni imewashirikisha wanawake kutoka pembe tofauti za mji huo.
Katika semina hiyo Bi Zainab Jumua mmoja wa wanafunzi waliohitimu masomo yao katika chuo cha masomo ya kidini cha Zahra (as) katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran na ambaye ni mwalimu katika Madrasa ya Darul Huda nchini Tanzania alizungumzia fadhila za kiakhlaqi, maisha na nafasi muhimu na tukufu ya Bibi Fatma (as) katika Uislamu. 1033558