Maadhimisho hayo ambayo yamepangwa kuanza saa nne mchana kwa wakati wa Uganda na kumalizika kabla ya swala ya adhuhuri yatahudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi, wanafikra na wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw).
Sheikh Suleiman Imam wa Msikiti wa Mashia wa Jinja aliyehitimu masomo yake katika chuo cha kidini cha Jamiatul Mustafa (saw) al-Alamiya nchini Iran anatarajiwa kuzungumza katika maadhimisho hayo kuhusiana na ghaiba ya muda mrefu ya Imam Mahdi (af) na majukumu ya Mashia katika kipindi hiki muhimu. 1041138