Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 5 Julai katika mji wa Orsay ulioko umbali wa kilomita 20 kutoka mjini Paris yatakamilika leo jioni.
Washiriki katika masomo hayo yanayosimamiwa na Baraza la Uhusiano wa Kitaifa na Waislamu la Ufaransa wanafundishwa misingi ya Uislamu, historia ya dini hiyo na sheria za Kiislamu. Makasisi hao pia watajadili njia za kuimarisha uhusiano baina ya Waislamu na Wakristo.
Mbali na makasisi wa Kanisa Katoliki kutoka maeneo mbalimbali ya Ufaransa, masomo hayo pia yanahudhuriwa na wawakilishi wa jumuiya na taasisi za kidini na pia jumuiya zinazozimamia mazungumzo kati ya dini mbalimbali kutoka nchi za Misri, Chad na Algeria. 1047352