IQNA

Haram Takatifu ya Karima Ahul Bayt (SA)

Fatima, mashuhuri kama Hadhrat Maasuma (SA) ni bintiye Imam Kahdim (AS) na dada yake Imam Ridha AS. Hadhrat Maasuma (SA) alikuwa na lakabu nyingine mashuhuri ya 'Karima Ahlul Bait'. 'Karima' ni neno lenye maana ya mwanamke mkarimu na mrehemevu.

Akiwa safarini nchini Iran kumtembelea ndugu yake, Imam Ridha AS, aliugua na akafariki dunia mjini Qum na akazikwa mjini hapo.