IQNA

Saudia yatangaza kuendelea kusitisha Ibada ya Umrah, misikiti yafunguliwa

15:57 - May 26, 2020
Habari ID: 3472803
TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia imesema itaendelea kusitisha kwa muda Ibada ya Umrah ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona lakini misikiti yote nchini humo imefunguliwa isipokuwa Msikiti Mtakatifu wa Makka.

Mapema mezi Machi Saudia ilitangaza kusitisha kwa muda Ibadah na Umrah baada ya kufunga misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina ikiwa ni katika jitihada za kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Wiki Saudia imetangaza itaanza kupunguza zuio la usafiri baina ya miji miezi miwili baada ya sheria kali kuwekwa ili kukabiliana na janga la COVID-19. Aidha msikiti yote Saudia itafunugliwa kwa muda wa siku 20 na waumini wametakiwa kuzingatia kanuni za afya zilizowekwa ili kuzuia kuenea corona.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Saudia (SNA),  kuanzia Juni 21 vizingiti vilivyowekwa vitaondolewa katika hatua tatu na kuishia kwa kuondolewa sheria ya kutotoka nje kote katika nchi hiyo isipokuwa katika mji mtakatifu wa Makka. Taarifa hiyo imesema Ibada ya Umrah, ambayo huwavutia mamilioni ya waumini kila mwaka kutoka maeneo yote ya dunia, itaendelea kusitishwa kwa muda usiojulikana. Waziri wa Hija wa Saudia pia amewataka Waislamu kwa sasa wasitishe mpango wa Ibada ya Hija hadi watakapokea maelekezo.

Idadi ya walioambukizwa COVID-19 nchini Saudia hadi kufikia sasa ni 74,795 na waliofariki ni 399.

3901306

Kishikizo: umrah saudia COVID-19
captcha