IQNA

Saudia yaendelea kupiga marufuku Umrah kutokana na COVID-19

18:14 - June 21, 2020
Habari ID: 3472885
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imetangaza kuwa hata baada ya amri ya kutotoka nje kufutwa kitaifa lakini marufuku ya Ibada ya Umrah itaendelea kutekelezwa.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Sky News Arabia, wizara hiyo imesema marufuku ya Umrah iliyotangazwa Machi kutokana na mlipuko wa COVID-10 itaendelea kutekelezwa.

Taarifa hiyo imesema hali ya Ibada ya Umrha itaendelea kutathminiwa kwa mujibu wa taarifa za afya kuhusu janga la COVID-19.

Saudi Arabia bado haijatoa tangazo la mwisho kuhusu kufanyika au kutofanyika Ibada ya Hija mwaka huu ingawa baadhi ya nchi kama vile Indonesia, India na Afrika Kusini zimetangaza kuwa raia wan chi hizo hawatashiriki katika Ibada ya Hija kutokana na janga la COVID-19.

3905861

Kishikizo: umrah hija covid 19
captcha