IQNA

Maandamano kote duniani kulaani ubaguzi wa rangi wa Polisi ya Marekani

Maandamano kote Marekani dhidi ya kitendo cha kinyama cha polisi mzungu kumuua George Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika katika mji wa Minneapolis yameendelea kwa wiki mbili nchini humo na sasa yamefuka mipaka na kuenea kote duniani katika nchi kama vile Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi, Austria, Uingereza, Lithuania, Mexico, Brazil, Canada, Japan, Korea Kusini, Australia, Mali, Tunisia na Uturuki. Waandamanaji ambao wamemiminika mitaano kwa malefu wanaunga mkono watu wenye asili ya Afrika Marekani huku wakilaani ubaguzi.