IQNA

Abdollahian: Trump ni gaidi nambari moja duniani

16:41 - October 31, 2020
Habari ID: 3473315
TEHRAN (IQNA) - Mshauri wa sera za kigeni wa Spika wa Bunge la Iran ameashiria mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye aliuawa kigaidi kufuatia amri ya rais Donald Trump wa Marekani na kusema, Trump ni gaidi nambari moja duniani.

Hossein Amir Abdollahian ameongeza kuwa Idara ya Mahakama ya Iran imewasilisha kesi kieneo na kimataifa kuhusu mauaji ya Shahidi Soleimani. Aidha amesema hafla za kumkumbuka Shahidi Soleimani zimefanyika kote duniani ikiwemo ndani ya Marekani kwenyewe kulikofanyika hafla za kumkumbuka jenerali huyo aliyepata umaarufu kutokana na kuongoza vita dhidi ya magaidi. 

 Akizungumza mjini Tehran katika kikao na waandishi habari kuhusu 'Kumbukumbu ya Mwaka Moja Tokea Auawe Shahidi Qassem Soleimani', Abdollahian amesema kuna filamu ya matukio ya kweli ambayo inaelekezea siku 14 za maisha ya Shahidi Soleimani ambayo itarushwa wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea auawe shahidi. 

Mnamo Januari 3 mwaka huu, jeshi la kigaidi la Marekani kwa amri ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump lilitenda jinai kwa kumuua kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran akiwa uraiani nchini Iraq tena akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Baghdad.

Katika jinai hiyo aliuawa shahidii pia Abu Mahdi al-Mohandes, Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu al-Shaabi pamoja na watu waliokuwa wamendamana nao. Tukio hilo lilitokea jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Jinai hiyo ya Marekani ilikabiliwa na ukosoaji mkubwa na kulaaniwa kimataifa. 

3932322

captcha