IQNA

0:09 - February 14, 2020
News ID: 3472469
TEHRAN (IQNA) - Marasimu ya maombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) yamefanyika Alhamisi kote nchini Iran kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa matabaka mbalimbali ya wananchi.

Kamanda shahidi Qassem Soleimani ambaye tarehe Tatu Januari mwaka huu alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq al Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la utawala wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad.  

Wananchi katika Iran nzima ya Kiislamu wameshiriki kwenye marasimu ya mombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake wengine na kusisitiza kuondoka wanajeshi magaidi wa Marekani katika eneo. 

Matabaka mbalimbali ya wananchi hapa nchini zikiwemo familia za mashahidi, baadhi ya maafisa wa serikali na jeshi pia walifika katika haramu tukufu za Imam Reza AS  huko Mash'had na kwa Bi Fatima Maasuma SA  katika mji mtukufu wa Qum na kuomboleza kifo cha shahidi Qassem Soleimani.

Arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani yafanyika kote nchini Iran

Marasimu ya arobaini ya Kamanda Soleimani na wanajihadi wenzake yatafanyika  Alhamisi alasiri  hapa Tehran na kuhutubiwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Katika hafla hiyo,  Kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Brigedia Jenerali Ismail Qaani amesoma wosia wa Shahidi Soleimani.

Wananchi katika miji mingine ya Iran ikiwemo Urumiye, Isfahan, Ilam, Mahabad, Ardabil, Birjand, Zahidan, Kerman, Shahr Kurd, Tabriz na Hamedan wamefanya kumbukumbu hii ya arobaini ambapo mbali ya kushukuru jibu kali lililotolewa na jeshi la IRGC kwa jinai za kigaidi za Marekani wamesisitiza juu ya kukabiliana vikali na njama zozote za utawala wa Marekani.

3878629

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: