IQNA

18:18 - January 06, 2020
News ID: 3472346
TEHRAN (IQNA) - Chama tawala cha ANC cha Afrika Kusini kimetoa taarifa rasmi na kulaani hujuma ya Jeshi la Markeani ambayo ilipelekea kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC)

Katika taarifa ANC imesema: "Kitendo hicho kisicho cha ubinadamu ni hujuma dhidi ya mamlaka ya kujitawala na uhuru wa watu wa Iran. ANC inapinga vikali hujuma hii ya wazi dhidi ya watu na serikali ya Iran. Hujuma hii inaweza kulitimbukiza eneo la Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) na dunia nzima katika vita." Taarifa hiyo imesema historia inaonyesha kuwa, waathirika wakubwa wa ugaidi kama huo wa Marekani ni wazee, watoto na wanawake huku vijana nao wakiathirika vibaya kutokana na kukumbwa na mustakbali mbaya. Taarifa hiyo ambayo imetiwa saini na katibu mkuu wa ANC Ace Magashule imesema: "ANC na harakati zote zipendazo maendeleo duniani haziwezi kunyamaza kimya wakati kwa vitendo vyake, Marekani inavuruga amani na usalama duniani  sambamba na kuvuruga kwa makusudi uthabiti wa kitaifa Iran." ANC imetoa wito kwa mataifa ya dunia, kupitia Umoja wa Mataifa kuchukua hatua imara kuzuia ugaidi wa kimataifa wa Marekani.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine nane, walishambuliwa kwa anga na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote walikufa shahidi katika tukio hilo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jumatatu asubuhi katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, amesalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC na mashahidi wenzake. Mamilioni ya wananchi wa Iran wameshiriki katika mazishi ya mashahidi hao.

Siku ya Jumamosi kulifanyika maandamano ya mazishi ya mashahidi hao katika miji ya Kadhimein, Baghdad, Karabala na Najaf nchini Iraq.

Mapema Jumapili miili mitoharifu ya mashahidi hao iliwasiliaAhavaz, mkoani Khuzestan, ambapo kulifanyika shughuli ya mazishi na kuwaaga mashahidi hao wa muqawama.

Baadaye  adhuhuri Jumapili shughuli ya mazishi iliendelea katika Haram Takatifu ya Imam Ridha AS, Imam wa nane wa Mashia katika mji wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran. Siku ya Jumatatu sala ya maiti ya mashahidi hao mashujaa ilisaliwa mjini Tehran (kama tulivyoashiria hapo juu)  na kisha shughuli ya mazishi ikaendelea katika mji wa Qum.

Maziko ya Shahidi Soleimani yamepengwa kufanyika katika mji alikozaliwa wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.

40075347

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: