IQNA

13:04 - February 02, 2020
News ID: 3472433
TEHRAN (IQNA)- Kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina na kuhakikisha kuwa ndoto zao za kuwa taifa huru zinafanikiwa.

Brigedia Jenerali Ismail Qaani amesema hayo katika mazungumzo yake ya simu na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniyah na Ziyad al-Nakhalah, mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Brigedia Jenerali Ismail Qaani aliyechukua nafasi ya Shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani aliyeuawa kigaidi na Marekani nchini Iraq mwanzoni mwa mwaka huu amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itasimama na Wapalestina bega kwa bega kuhakikisha kuwa njama za Marekani zinazolenga kukanyaga zaidi haki zao kwa jina la 'Muamala wa Karne' zinaporomoka.

Amewahakikishia wakuu hao wa harakati za Muqawama za Palestina kuwa, hakuna chochote kilichobadilika katika sera za Iran za kuwaunga mkono Wapalestina hususan baada ya kuuawa shahidi Jenerali Soleimani.

Kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani ilitekeleza ugaidi wa kumuua shahidi Soleimani kama sehemu ya maandalizi ya kuzindua mpango wake huo batili wa 'Muamala wa Karne."

Wakuu hao wa harakati za Muqawama za Palestina wamelishukuru taifa la Iran kwa kuendelea kuwanga mkono Wapalestina kwa hali na mali katika kupambana na njama za madola ya kiistikbari yanayopania kubadilisha utambulisho na nembo za matukufu ya Kiislamu.

4841726

Tags: iqna ، quds ، IRGC ، QAANI ، HAMAS ، jihad islami
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: