IQNA

Trump ajaribu kufunika udhaifu wa Marekani baada ya jibu kali la Iran

20:53 - January 09, 2020
Habari ID: 3472357
TEHRAN (IQNA) - Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza kivitendo ahadi yake ya kutoa jibu kali kwa jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC

Katika majibu hayo makali, Iran imepiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za  kijeshi za Marekani za Ain al Asad na Erbil nchini Iraq. Licha ya kwamba huko nyuma rais wa Marekani, Donald Trump alitishia kutoa majibu makali iwapo Iran itajibu jinai za Washington, lakini msimamo wa Marekani umebadilika kabisa baada ya majibu makali yaliyotolewa na Iran.

Mara baada ya Marekani kumuua kigaidi na kidhulma Luteni Jenerali Soleimani, vyombo vya habari vya nchi hiyo na vya Magharibi viliendesha propaganda kubwa ya vita vya kisaikolojia huku rais wa Marekani akitoa vitisho kwamba atapiga vituo 52 muhimu vya Iran, vya kiutamaduni, kisiasa, kijeshi, kiuchumi n.k, kama Iran italipiza kisasi. Lakini baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuipiga Marekani kibao kikali cha uso, viongozi wa White House wameshindwa kuficha kutapatapa kwao na baada ya kuchukuka muda mrefu na kuakhirisha mara kadhaa hatimaye Donald Trump jana jioni alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kurudia tuhuma zile zile za kila siku dhidi ya Iran, akatoa ahadi zile zile za kila siku za kuiwekea vikwazo zaidi Iran na hakuzungumzia kabisa vitisho alivyotoa siku chache tu zilizopita.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, lengo la Trump la kurudia tuhuma za huko nyuma na kutozungumzia kabisa vitisho alivyotoa, ni kujaribu kuonesha kuwa, kipigo cha makombora kilichotolewa na Iran kwenye kambi za kijeshi za Marekani huko Iraq hakina umuhimu wowote. Trump amedai pia kwamba, hakuna Mmarekani hata mmoja aliyepata madhara kwenye mashambulizi hayo ya Iran, bali kuna hasara chache tu zimetokea katika kambi hizo. Madai hayo yametolewa katika hali ambayo, duru za ndani ya Iraq kwenyewe zinasema kuwa, makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC yamezisababishia kambi hizo mbili hasara kubwa na kwa uchache wanajeshi 80 wa Marekani wameangamizwa na wengine karibu 200 wamejeruhiwa.

Trump amefanya makusudi kutoa madai hayo ili kukimbia kipigo kingine kikali zaidi kutoka kwa Iran kwani Jamhuri ya Kiislamu imeonya kuwa, iwapo Marekani itajibu, basi utawala wa Kizayuni wa Israel hautosalimika, bali nchi yoyote itakayotoa ardhi yake kutumiwa na Marekani kushambulia Iran, basi hiyo nayo itahesabiwa kuwa ni adui wa taifa hili na haitosalimika na vipigo vya Iran.

Inavyoonekana ni kwamba, rais wa Marekani, Donald Trump ambaye kipindi chote cha uongozi wake amekitumia kutoa vitisho kwa nchi nyingine hasa Iran, na hivi sasa anaendeleza siasa za kuiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha juu zaidi kwa tamaa kwamba atawalazimisha viongozi wa Tehran kuipigia magoti Washington, alitoa vitisho vingine kwa Iran ili isijibu jinai yake ya kumuua kidhulma na kigaidi, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wenzake. Hata hivyo suala ambalo Trump amekwepa kwa makusudi kuligusia katika hotuba yake ya jana, ni vitisho vyake alivyovitoa hivi karibuni kabisa dhidi ya Iran wakati alipojigamba kuwa atashambulia maeneo 52 muhimu mno ndani ya Iran.

Alaakullihaal, katika hotuba yake ya dakika chache aliyoitoa jana Jumatano, Trump aliishia kukariri tuhuma za huko nyuma tu dhidi ya Iran. Upinzani mkali wa hata ndani ya Marekani kwenyewe wa kupinga vita na Iran na onyo kali la madhara makubwa yatakayopatikana iwapo Marekani itaingia vitani na Iran yamemtia kiwewe Trump.

Harry Kazianis mkurugenzi wa mitengo cha utafiti wa kiulinzi cha chuo cha Marekani kinachoitwa "Kituo cha Manufaa ya Taifa" amesema, mashambulizi ya Iran kwenye kambi za kijeshi za Marekani huko Iraq ni onyo kwa Donald Trump kwamba Iran ni dola kubwa la makombora duniani leo hii.

Jambo jingine lililofanywa na Trump katika hotuba yake ya jana ni kurudia tuhuma zake za kila siku kwamba eti Iran inafanya juhudi za kumiliki silaha za nyuklia. Ni jambo lililo wazi kwamba lengo la kurudia tuhuma hizo ni katika juhudi zake Trump za kupotosha fikra za walimwengu ili wasione udhaifu wa Marekani wa kutothubutu kujibu kibao cha uso walichopigwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

180295

captcha