IQNA

Siku ya Kimataifa ya Msikiti

TEHRAN (IQNA)- 21 Agosti inatambuliwa kama siku ya kimataifa ya msikiti kwa mnasaba wa kukumbuka tukio chungu la Agosti 21, 1969 wakati Mzayuni Michael Dennis Rohan alipoitekteza moto sehemu ya Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Upasishwaji wa siku hii ulijiri mwaka 1382 Hijiria Shamsia, sawa na tarehe 22 Agosti mwaka 2003 Miladia katika mkutano uliofanyika mjini hapa Tehran na kwa pendekezo la Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la nchini Iran (ICRO) sanjari na kupitishwa na Wizara za Mashauri ya Kigeni za nchi za Kiislamu. Kikao hicho kilifanyika kwa mnasaba wa wiki ya kumbukumbu ya kuchomwa moto msikiti wa Al-Aqsa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel tarehe 21 Agosti mwaka 1969 katika mji wa Quds (Jerusalem). Aidha katika kikao hicho nchi za Kiislamu zilitakiwa kutoa himaya kwa misikiti kama mahala patakatifu sanjari na kuienzi sehemu hiyo.

 
 
Kishikizo: msikiti