IQNA

Haram ya Al-Kadhimayn nchini Iraq

Msikiti wa Al Kadhimiya au Haram ya Al Kadhimiya katika eneo la Kadhimayn kaskazini mwa Baghdad ina makaburi mawili ya Imam Musa Kadhim AS na Imam Jawad AS, Maimamu wa Saba na Kumi wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia.

Leo ni Jumapili tarehe 25 Rajab 1443 Hijria sawa na Februari 27 mwaka 2022. Siku kama ya leo miaka 1260 iliyopita, Imam Musa Kadhim AS mmoja wa wajukuu watoharifu wa Mtume Muhammad SAW aliuawa shahidi. Imam Kadhim SAW alizaliwa mwaka 128 Hijiria huko katika eneo la Ab'waa lililoko baina ya miji mitakatifu ya Madina na Makka.