TEHRAN (IQNA)- Kaburi la Nabii Danieli liko katika mji wa Shush au Shushani, kusini magharibi mwa Iran na lina muundo wa kipekee miongoni mwa maeneo ya kidini kote Iran.
Kaburi hilo lina umuhimu na utukufu wa kipekee kwa wakazi wa eneo hilo na ni moja ya vivutio vya kitalii katika mji wa Shush mkoani Khuzeshtan.