Dua na kutawasali ni miongoni mwa hali bora za kiroho za mwanadamu, ambazo huongeza daraja za kiroho za mwanadamu na kumuwezesha kubainisha mahitaji yake kwa Mola Muumba.
Kila ibada ina mila na masharti ambayo bila hiyo haitakuwa na ufanisi. Moja ya desturi za dua ni kuchagua wakati na mahali sahihi, na Ramadhani ni moja ya nyakati bora katika suala hili, na Dua ya Al-Iftitah au "maombi ya kufungua" pia ina mada zinazopendekezwa kusomwa katika usiku wa Ramadhani.
Dua hii huanza kwa maneneo yafuatayo: «اللهمَّ انِّی افْتَتِحُ الثَّناءَ بِحَمْدِکَ "Ewe Mungu wangu! Hakika mimi naanza kukutukuza kwa hamdi Yako".
Kwa hivyo mja huanza kwa kumtukuza Mola Muumba. Sehemu nyingine ya dua hiyo tunasoma
الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِی یُؤْمِنُ الْخَائِفِینَ وَ یُنَجِّی [یُنْجِی] الصَّالِحِینَ
" Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu, ambaye huwapa amani wenye hofu. Huwaokoa waja wema. Huwanyanyua waliodhoofishwa.
Pia tunasoma katika dua hii:
اسْتَجِبْ بِهِ دَعْوَتَنا وَ اَعْطِنا بِهِ سُؤْلَنا و بَلِّغْنا بِهِ مِنَ الدُّنْیا وَ الْأَخِرَةِ امالَنا و اَعْطِنا بِهِ فَوْقً غْبَتِنا یا خَیْرَ الْمسؤلینَ؛
Tujibu dua yetu na tupe maombi yetu. Tutimizie matarajio yetu duniani na Akhera. Na utupe zaidi ya mategemeo yetu. Ewe mbora wa waombwaji.
Sehemu ya kwanza ya dua hii inahusu kumjua Mwenyezi Mungu na inaelezea sifa zinazoonyesha sehemu ya ukuu Wake. Sehemu ya pili ya dua hii ni salamu na baraka kwa Mtume (SAW) na kizazi chake kotaharifu na kielelezo cha nafasi yao muhimu na ukamilifu. Sehemu ya tatu ya dua hii ya ufunguzi inahusiana na Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake), dua ya kuja kwake na matakwa ya kusimamisha serikali ya haki na utawala wa haki.
Katika sehemu ya Dua ya Al-Iftitah tunaseoma:
«اَللَّهُمَّ اِنّا نَشْکُو اِلَیْکَ فَقْدَ نَبِیّنا صَلَواتُکَ عَلَیْهِ وَ آلِهِ وَ غَیْبَة وَ لِیِّناَ وَ کَثرَةَ عَدُوِّنا و قِلّةَ عَدَدِنا وَ شِدَّةَ الْفِتَن بِنا و تَظاهُرَ الزَّمانِ عَلَیْنا
"Ewe Mungu wangu! Hakika sisi tunakushtakia kutoweka kwa Mtume wetu, rehema Zako ziwe juu yake na juu ya kizazi chake, ghaiba ya walii wetu na uwingi wa maadui zetu, uchache wa idadi yetu na ukali wa fitina kwetu, na ushindi wa zama dhidi yetu."