IQNA

Rais wa Iran katika mazungumzo na Bin Salman wa Saudia

Maadui walilenga kuigeuza Iran kuwa Syria au Libya nyingine

8:55 - January 28, 2026
Habari ID: 3481858
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni, maadui, yaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, walilenga kuigeuza Iran kuwa Syria au Libya nyingine,"

Rais Pezeshkian alitoa matamshi hayo jana jioni katika mazungumzo ya simu na  Mwanamfalme Mrithi wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Rais wa Iran ameonya kwamba harakati za kijeshi za Marekani na matamshi yake katika Asia Magharibi ni sehemu ya juhudi zilizopangwa za kuyumbisha amani ya eneo hilo.

“Vitisho na operesheni za kisaikolojia za Marekani zinalenga kuvuruga usalama wa eneo la Asia Magharibi na hazitafanikisha chochote zaidi ya kuhatarisha amani,” Pezeshkian amemwambia Mwanamfalme Bin Salman.

Matamshi hayo yanajiri kufuatia kuwasili kwa meli ya kubeba ndege ya Marekani katika eneo hilo, sambamba na kuongezeka kwa vitisho kutoka Washington.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Rais Pezeshkian ameashiria kuongezeka kwa uadui wa Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Iran tangu kuanza kwa muhula wake wa uongozi.

Ametaja mashinikizo ya kiuchumi, Vita vya Siku 12 dhidi ya Iran, pamoja na kuhusika moja kwa moja kwa Marekani na washirika wake katika kuchochea ghasia za hivi karibuni za kigaidi ndani ya Iran. Ghasia hizo zilisababisha mauaji ya raia na maafisa wa usalama, pamoja na uharibifu mkubwa wa mali ya umma, ikiwemo masoko na misikiti.

08:55 - 2026/01/28

“Walidhani wangeweza kuigeuza Iran kuwa Syria au Libya nyingine,” amesema Rais Pezeshkian, akisisitiza kuwa, “walishindwa kutambua uhalisia, asili na ukubwa wa taifa la Iran. Ushiriki wa wananchi wetu katika medani uliishinda njama yao.” Kauli hiyo ilirejelea maandamano makubwa ya mamilioni ya Wairani waliopinga ghasia hizo kote nchini katika wiki zilizopita.

Mapema mwezi huu, Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuishambulia Iran iwapo, kwa madai yake, ingewaua aliowataja kuwa “waandamanaji wa amani”.

Siku chache baadaye, Januari 8 na 9, makundi ya kigaidi, yakipata himaya ya Marekani na Israel, yalianzisha wimbi la mashambulizi ya silaha dhidi ya vituo vya polisi, kambi za kijeshi na maeneo mengine nyeti, ikiwemo miundombinu ya raia, katika miji kadhaa nchini Iran.

Maafisa wa Iran wamesema mashambulizi hayo ya vurugu yalikusudiwa kusababisha vifo vya watu wengi na kuvuruga utulivu katika miji mbalimbali kote nchini.

Habari inayohusiana:

Vilevile, wamekosoa mara kwa mara vyombo vya habari vya Magharibi kwa kusambaza ripoti nyingi za uongo kuhusu idadi ya waliouawa katika ghasia hizo, pamoja na propaganda za kuhusisha serikali ya Iran na vifo hivyo.

Iran pia imeonya kuwa Jamhuri ya Kiislamu itatoa “jibu la kutisha” kwa kitendo chochote cha uchokozi, ikisisitiza kuwa taifa hilo sasa lina uwezo mkubwa zaidi wa kijeshi kuliko wakati wowote uliopita.

4330721

captcha