IQNA

Mwanaharakati wa Iran atoa wito wa kuundwa Jumuiya ya Kimataifa ya Maqari wa Qur’ani

14:15 - January 27, 2026
Habari ID: 3481856
IQNA – Akilaani matukio ya hivi karibuni ya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu, mwanaharakati wa Qur’ani kutoka Iran ametoa wito wa kuundwa kwa Jumuiya ya Kimataifa wa Maqari wa Qur’ani ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kufuatilia hatua za kisheria dhidi ya vitendo hivyo.

Sayyid Abbas Anjam, katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), amesema kuwa, “Hatua kama kutoa taarifa au kufanya maandamano ya kupinga udhalilishaji wa Qur’ani ni muhimu, lakini kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya mashambulizi ya maadui kunahitaji chombo rasmi zaidi, kama uJumuiya ya Kimataifa wa Maqari wa Qur’ani.”

Akirejea machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yaliyoungwa mkono na tawala za kigeni, ambapo misikiti na nakala za Qur’ani zilidhalilishwa, alisema matukio hayo machungu, hususan udhalilishaji wa Qur’ani na mashambulizi dhidi ya maeneo matukufu, ni ishara ya chuki ya maadui dhidi ya Uislamu, dhidi ya Iran, na bila shaka dhidi ya Ushia; jambo ambalo si jipya na halitaisha kwa tukio hili pekee. Aliongeza kuwa, “Hakuna shaka kuwa adui anaandaa mipango mingine mibaya kuendeleza dharau na uhasama.”

Sayyid Anjam alibainisha kuwa kile kinachofanya mashambulizi haya yaonekane wazi zaidi katika matukio ya karibuni ni kwamba, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, uhasama huu sasa umejitokeza waziwazi; kwa maneno mengine, adui amechomoa upanga wake dhidi ya kila kitu kinachohatarisha uwepo na nafasi yake.

Habari inayohusiana:

Alisifu pia msimamo wa wananchi wa Iran kulaani mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni, akisema kuwa hatua hiyo inaonyesha uhusiano wa kina wa watu na Qur’ani pamoja na neno la wahyi.

Alisisitiza kuwa kila mtu anapaswa kuimarisha uhusiano wake na Qur’ani. “Hakika, wakati huu haitoshi tena kuisoma Qur’ani tu; bali kupitia usomaji, lazima tufikie hatua ya kuelewa ili tuweze kutenda kwa mujibu wa mafundisho yake.”

3496196

captcha