
Harakati ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imesema katika taarifa yake ya Jumapili usiku kwamba inawatolea wito wale wote wenye nia ya kupambana kujiandaa kwa ajili ya vita kubwa ya kuuinga mkono Iran dhidi ya "harakati ya ukafiri na unafiki".
Kata'ib Hizbullah imesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ngome na chimbuko la fahari ya Umma wa Kiislamu ambayo imesimama pamoja na wanaodhulumiwa kwa zaidi ya miongo minne sasa, bila kujali madhehebu, rangi au utaifa wao.
Taarifa ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imevitaja vitisho vinavyoendelea kutolewa dhidi ya Iran kuwa jaribio la pande potofu, ikiwa ni pamoja na Wazayuni na madhalimu kwa lengo la kuitisha au kuharibu nchi na kudhoofisha thamani za kimaadili duniani kote.
Harakati hiyo ya muqawama ya Iraq imewataka mujahideen wote wa mashariki na magharibi mwa dunia waliojaa imani na wanaopinga harakati ya ukafiri na unafiki kujiandaa kwa ajili ya kuiunga mkono kikamilifu Iran.
Habari inayohusiana:
Taarifa ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imewaonya maadui wa Iran kwamba vita vyovyote dhidi ya nchi hiyo havitakuwa rahisi, na wataonja aina zote za kifo cha ghafla na wataangamizwa katika eneo la Asia Magharibi.
Harakati ya Hizbullah ya Iraq imeeleza hayo kufuatia kuongezeka mvutano kati ya Iran na Marekani baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutishia kutumia nguvu ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
3496184