IQNA

Waziri wa Awqaf Algeria awakabidhi wanazuoni wa Afrika nakala ya Qur'ani ya kihistoria

16:30 - January 26, 2026
Habari ID: 3481851
IQNA – Waziri wa Mambo ya Dini na Awqaf wa Algeria amewakabidhi wanazuoni wa Afrika nakala ya kihistoria ya Qur'ani Tukufu ijulikanayo kama “Rhodosi”, wakati wa kongamano lililofanyika nchini humo kuhusu diplomasia ya kidini.

Youssef Belmahdi, katika kikao maalumu na wanazuoni na wasomi walioshiriki katika kongamano la “Diplomasia ya Kidini katika Ukanda wa Sahel ya Afrika”, aliwakabidhi nakala hiyo adhimu ya Rhodosi, ambayo ilichapishwa chini ya usimamizi wa Rais Abdelmadjid Tebboune.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya dini ya Algeria, kikao hicho kilifanyika mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, gazeti la Al-Ittihad liliripoti.

Kongamano hilo liliandaliwa na Jumuiya ya Wanazuoni, Waalimu wa Dini na Maimamu wa Nchi za Ukanda wa Sahel kwa ushirikiano na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Algeria.Katika mkutano huo uliowakutanisha washiriki kutoka nchi kumi na moja za Afrika, mada muhimu zilijadiliwa, ikiwemo nafasi ya diplomasia ya kidini katika kuimarisha usalama na uthabiti, kutatua migogoro katika eneo la Sahel, mchango wa Algeria katika kusuluhisha migogoro barani Afrika, pamoja na namna ya kukabiliana na tamaa za mataifa ya nje juu ya rasilimali za bara hilo.

Moussa Sarr, mwakilishi wa Mauritania katika Jumuiya ya Wanazuoni wa Sahel, alisisitiza umuhimu wa kuhuisha diplomasia ya kidini kama nyenzo ya kupambana na vurugu na misimamo mikali. Pia alieleza kuwa kongamano hili lina mchango mkubwa katika kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa mbinu hii ya kidiplomasia katika kulinda amani na mshikamano wa kijamii.

Habari inayohusiana:

Alisema kuwa mbinu za jadi pekee hazitoshi tena kukabiliana na misimamo mikali na ugaidi; badala yake, kunahitajika mkabala wa kidini unaoweza kugusa mizizi ya tatizo hili. Qur'ani ya Tha‘alibiyya, inayojulikana pia kama Qur'ani ya Rhodosi, ni nakala ya kihistoria ya Algeria iliyoandikwa kwa riwaya ya Warsh kutoka kwa Nafi‘, kwa hati ya Kimaghrib. 

Uchapishaji wake ulianza mwaka 1350 Hijria, sawa na 1931 Miladia.Dar al-Tiba‘a al-Tha‘alabiyya ndicho kituo kilichochapisha nakala ya kwanza ya Qurani Tukufu nchini Algeria mwaka 1931.

Nakala hiyo iliandikwa kwa hati ya Kimaghrib na marehemu mwandishi na mpambaji wa maandishi, Muhammad Sharadi, maarufu kama Muhammad al-Safti au Muhammad al-Safati, kwa mujibu wa riwaya ya Warsh kutoka kwa Nafi‘.

4330227

captcha