IQNA

Hizbullah yasema haitakaa kimya mbele ya uchokozi wowote dhidi ya Iran

11:53 - January 27, 2026
Habari ID: 3481853
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa: "Imam Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni Faqihi Mtawala wetu na sisi hatutabaki kuwa watazamaji mbele ya uchokozi wowote utakaofanywa dhidi ya Iran".

Sheikh Naim Qassem, ameyasema hayo alipohutubia mkutano wa mshikamano wa wananchi wa Lebanon na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wa kulaani za kumvunjia heshima Imam Khamenei, mkutano ambao ulifanyika jana Jumatatu katika Uwanja wa Sayyidu-Shuhadaa.

Amesema: "tumekusanyika hapa kutangaza mshikamano na usaidizi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kiongozi wake anayetupa ilhamu, Imam Sayyid Ali Khamenei. Ninatoa mkono wa kheri na baraka kwa Waislamu wote kwa kuandama mwezi wa baraka wa Sha'bani. Mwezi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, mwezi wa kuzaliwa Maimamu na mwezi wa maandalizi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kwetu sisi, Imam Khamenei ni Faqihi Mtawala, Kiongozi Mshika Hatamu katika kipindi cha kughibu Imam Mahdi AS, na Naibu wa Imam huyu maasumu, na tunaamini katika uongozi wa Faqihi Mtawala.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kwa kusema: Hatutabaki kuwa watazamaji mbele ya uchokozi wowote dhidi ya Iran.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amebainisha katika hotuba yake kwa kusema: Tangu ilipoasisiwa Jamhuri ya Kiislamu, Marekani ilianza kukabiliana nayo, na ikaanzisha dhidi yake vita vya miaka minane kupitia Iraq.

Habari inayohusiana:

Sheikh Naeem Qassem ameongezea kwa kusema: sisi tunatuma salamu kwa Jamhuri ya Kiislamu na tunasema tunajivunia kwayo, na pia tunamwambia Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba tuko pamoja nawe daima. Imam Khamenei ndiye anayetutawalia mambo wetu na kiongozi wetu, na kitisho chochote dhidi yake kinamaanisha kutoa kitisho dhidi ya makumi ya mamilioni ya watu. Wakati Trump anapotoa kitisho dhidi ya Imam Khamenei, huwa ni kama ametoa kitisho kwa makumi ya mamilioni ya watu wanaomfuata (Imam Khomeini). Sisi tuna wajibu wa kukabiliana na kitisho hiki kwa utayarifu na kwa nguvu zetu zote, kwa sababu shambulio lolote dhidi ya Imam Khamenei ni sawa na kutishia utulivu na hali katika eneo hilo na ulimwengu mzima, kwa sababu wafuasi na wapenzi wa Faqihi Mtawala wameenea (kila mahala).

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah ameeleza bayana kwamba, tangu mwaka 1979, Marekani imekuwa ikikabiliana na Jamhuri ya Kiislamu kwa sababu haiwezi kuvumilia kuwepo kwa nchi huru na inayojitawala kikweli na ambayo ni marejeo kwa Waislamu na wanaonyongeshwa duniani.

3496197

captcha