
Ayatullah Sheikh Isa Qassim alitoa kauli hiyo akijibu vitisho vipya vya Rais wa Marekani, Donald Trump, dhidi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, vitisho ambavyo vimeibua ukosoaji mpana katika eneo na duniani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Jumuiya ya Al‑Wefaq ya Bahrain katika mtandao wa X, Sheikh Qassim alisema sera za rais wa Marekani, zinazojengwa juu ya ubabe na matumizi ya nguvu za kimaada, zimeweka hatarini amani na usalama wa kimataifa. Aliongeza kuwa mataifa na serikali nyingi duniani, bila kujali msimamo wao kuhusu Marekani, sasa zinahofia mustakabali wao kwa sababu sera hizo hazizingatii mantiki, dini, wala maadili, na zimezua tishio kubwa kwa usalama wa dunia.
Alizitaja sera za Washington kuwa “njia ya uharibifu na ubabe,” akisisitiza kwamba madai ya Marekani kuhusu kuunga mkono mataifa na kuheshimu uhuru wa nchi nyingine hayana ukweli wowote. Alisema vitendo vya kijeshi kama vita vya siku 12 dhidi ya Iran mnamo Juni 2025 na vitisho vya mashambulizi mapana zaidi vinaonyesha wazi kuwa shabaha ni taifa la Iran lenyewe, si kulinda haki au maslahi yake.
Habari inayohusiana:
Ayatollah Qassim aliendelea kueleza nafasi ya kielimu, kiroho na kisiasa ya Ayatullah Khamenei kama ya kipekee na isiyo na mfano, akisema kwamba mamilioni ya watu wanamfuata kwa moyo wa dhati.
Aliongeza kuwa Ayatullah Khamenei ni mwakilishi wa dini na usalama wa Ummah wa Kiislamu, na kwamba kumlinda ni sawa na kulinda Uislamu na haki za binadamu.
Katika hitimisho lake, alisisitiza kwamba nafasi na uongozi wa Imam Khamenei ni muhimu si tu kwa Iran, bali pia kwa usalama, amani na ustawi wa dunia nzima.
3496213