
Maonyesho haya, ambayo yamepewa hadhi ya tukio la kipekee la kitamaduni, yamefuatilia historia ya uandishi wa Qur'ani katika vipindi mbalimbali vya ustaarabu wa Kiislamu, yakionesha safari yake kutoka Mashariki hadi Magharibi, na kutoka Asia ya Kati hadi Andalusia.
Maonyesho hayo, ambayo yataendelea hadi mwisho wa mwezi huu, yanawapa wageni fursa ya kufahamu mabadiliko ya hati za Qurani, kuanzia hati za awali za Kufi hadi Naskh, Thuluth, Diwani na Qur'ani zilizochapishwa, pamoja na kuangazia utofauti wa mapambo na ubunifu uliotokana na mazingira ya kisiasa na kitamaduni ya kila zama.
Maonyesho ya Qur'ani Adimu ni tukio jipya katika uwanja wa utamaduni wa Istanbul; jiji linalotazamwa kama kitovu cha urithi wa Kiislamu na mahali pa mikusanyiko ya kitamaduni inayounganisha historia na ulimwengu wa sasa.
“Maonyesho haya yanajumuisha jiografia ya Uislamu katika sehemu moja na yanaonesha namna Qurani, licha ya tofauti za lugha na tamaduni, imekuwa kiungo cha kuwaunganisha watu,” alisema Osman Onlu, mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki, katika mkutano na wanahabari.
Habari inayohusiana:
Akaongeza kuwa utofauti wa hati na mapambo katika nakala hizo unaonesha shule nyingi za sanaa, huku ukisisitiza uimara na umoja wa maandishi ya Qurani katika vipindi vyote vya historia.
Onlu alibainisha pia kuwa maonyesho hayo hayajikita tu katika upande wa sanaa, bali yanaakisi heshima na umakini mkubwa ambao Qurani Tukufu imepewa katika historia, na kuonesha namna Qurani, kama maandishi matukuf, imekuwa kitovu cha elimu na sanaa za Kiislamu, na daraja la kuwaunganisha mataifa ya Kiislamu licha ya tofauti zao za lugha na tamaduni.
4330175