IQNA

Mnong'ono wa Fajr /3

Usomaji wa "Surah Fajr" kwa sauti ya Abdul Basit

Katika riwaya tofauti, Maimamu wa Masoomin (AS) wamehusisha Sura ya “Alfajiri iliyobarikiwa” na Imam Hussein (a.s.); Kwa msingi kwamba mwamko wa Imamu huyo kulijiri wakati wa giza na kwa harakati yake aliibua Alfajiri mpya ambayo ni chanzo cha maisha mapya.

Katika mwezi wa Muharram na katika siku za maombolezo ya mashahidi wa Hadhrat Aba Abdullah Al-Hussein (AS), IQNA  imesambaza kisomo cha Surah Al Fajr kwa sauti za wasomaji mashuhuri duniani. Katika sehemu ya tatu, utasikia kisomo cha Surah Fajr kwa sauti ya Abdul Basit Muhammad Abdul Samad, msomaji maarufu katika ulimwengu wa Kiislamu.