IQNA

Hija 1445 katika Picha: Mamilioni wakusanyika kwenye Mlima Arafa

IQNA - Mamilioni ya mahujaji wa Kiislamu jana walikusanyika katika Mlima Arafa, karibu na Makka, kuashiria kilele cha Hija mwaka huu wa 1445 (2024).

Ukiwa unajulikana kam 'mlima cha rehema,' Mlima Arafat ni eneo la khutba ya  Kuaga ya Mtume Muhammad (SAW), iliyotolewa miaka 1,435 iliyopita, ambapo alizungumzia usawa na umoja kati ya Waislamu.

Safari ya kuelekea mlima huo ulioko kilomita 20 kusini mashariki mwa Makka, ilianza mapema kabla ya mapambazuko, huku mahujaji wakitembelea umbali huo kwa miguu. Hisia zilienea sana miongoni mwa waumini huku wakiinua mikono yao katika dua, wengi wakibubujikwa na machozi, wakitafuta rehema, Baraka za Mwenyezi Mungu..