Matembezi ya Arbaeen ya ‘Walioachwa nyuma’ yafanyikaTehran
IQNA - Idadi kubwa ya waombolezaji walishiriki katika matembezi yaliyofanyika katika mji mkuu wa Iran wa Tehran Jumapili asubuhi, siku ya Arbaeen.
Katika msafara huo, wale wanaojulikana kana kama "walioachwa nyuma" (kwa kukosa fursa ya kushiriki katika maandamano ya kila mwaka ya Arbaeen nchini Iraq), walitembea kilomita kadhaa kutoka sehemu mbalimbali za Tehran hadi Rey, kusini mwa mji, huko Arbaeen.