Miaka 46 iliyopita yaani tarehe 13 Aban mwaka 1357 Hijria Shamsia (sawa na Novemba 4, 1979), kulifanyika maandamano makubwa ya wanafunzi na wanachuo mjini Tehran, kulalamikia njama kadhaa wa kadhaa zilizokuwa zikifanywa na Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.