IQNA

Jumbo la Makumbusho la Al-Kafeel katika Haram ya Hadhrat Abbas (AS)

IQNA – Makumbusho ya Al-Kafeel ya Hazina na Hati, ambayo iko ndani ya Haram ya Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala, Iraq, imejitolea kuhifadhi na kuonyesha turathi ya Kiislamu na mabaki ya kitamaduni. Makumbusho haya yanahifadhi mkusanyo mkubwa wa hati adimu, mabaki ya kihistoria, na hazina za thamani, ikiwa ni pamoja na sarafu za kale, nguo, na vyombo vya kauri.