IQNA- Katika dunia ya leo yenye pilika pilika nyingi na mwendo wa haraka, wakati mwingine tunahitaji kusimama kwa muda mfupi na kupata utulivu. Mfululizo wa "Sauti ya Wahyi" kwa kuchagua baadhi ya aya kwenye Qur'ani Tukufu na sauti ya kupendeza ya Ustadh Behrouz Razawi, ni mwaliko wa safari ya kiroho na yenye kuinua roho. Mfululizo huu mfupi lakini wenye maudhui ya kina, unawaletea nyakati za utulivu na matumaini.
Sura An Nahl aya za 52-55
وَلَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَهُ الدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ اللَّهِ تَتَّقُونَ
*Na ni vyake Yeye viliomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je! Mtamcha mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu? 52
وَمَا بِكُمْ مِنْ نِعْمَةٍ فَمِنَ اللَّهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ
*Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni madhara mnamyayatikia Yeye. 53
ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنْكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِنْكُمْ بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ
*Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi, 54
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ
*Wakizikataa neema tulizo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua! 55