IQNA

Mazuwari wa Arbaeen katika eneo la Bayna al-Haramayn mjini Karbala

IQNA – Pamoja na kuwasili kwa mazuwari au wafanyaziara wa Arbaeen katika mji mtakatifu wa Karbala, eneo la Bayna al-Haramayn, lililopo kati ya maeneo mawili matakatifu walimozikwa Imam Hussein (AS.) na Hadhrat Abbas (AS), ni miongoni mwa maeneo ya jiji hilo yanayoshuhudia misururu mikubwa ya mazuwari.