IQNA

Ujumbe wa Wahyi / 6

Tanbihi | Msifanye Khiyana

IQNA-Qur’ani Tukufu, kitabu cha mwongozo na mwamko wa mwanadamu, katika aya zake inawasilisha ujumbe ulio wazi na wenye kutoa mwanga kwa nyakati zote na kwa wanadamu wote; jumbe hizi zinajumuisha kila kitu kuanzia utunzaji wa imani na maadili ya mtu binafsi, hadi kusimama imara katika dhiki, kuwa na matumaini kwa rehema za Mwenyezi Mungu, uwajibikaji katika jamii, kuepuka kughafilika, na kusonga mbele katika njia ya haki. Mfululizo huu wa “Ujumbe wa Wahyi,” kwa kuchagua aya zenye mada maalum, unajitahidi kujenga daraja dhahiri kati ya dhana kuu za wahyi na maisha ya sasa ya wasomaji, huku ukiweka kila aya mbele ya msomaji kama ujumbe wenye kuhamasisha, wenye kutoa nafasi ya kutafakari, na wenye manufaa ya kiutendaji.

یَا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ‌ 

Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume...Al Anfal 27

پیام وحی