Vikao vya Itikafu Katika Haram ya Imam Ridha (AS) Mjini Mashhad, Iran
IQNA –Ibada ya Itikafu (kujitenga kwa ajili ya ibada msikitini) katika mwezi wa Rajab kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria imefanyika kuanzia Jumamosi asubuhi hadi Jumatatu jioni katika misikiti na maeneo matukufu kote Iran.
Picha zilizopigwa zinaonyesha ibada za Itikaf zikifanyika katika haram tukufu ya Imam Reza (AS) mjini Mashhad, ambapo waumini wamekusanyika kwa unyenyekevu na sakina, wakijitenga na dunia ili kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu.